Wednesday 9 October 2013

Hela za kupata uzeeni hizi..???

Wednesday, October 09, 2013 No comments


Bi mkubwa mmoja aliokota hela na kuamua kwenda kwenye show room ya
magari ili aweze kununua.
Basi alipofika ndani humo akaanza kuangalia ni gari lipi
linalompendeza ili aweze kununua,ndipo alipoliona Mercedes Benz macho
ya panzi akainama ili aziangalie vizuri Rim za gari hilo mara ghafla
akajamba,kitendo hiki kilimnyima raha ikabidi ageuke nyuma ili
kuangalia kama kuna mtu aliyestukia kama yeye kajamba,alipogeuka
akakutana na sura ya mfanyakazi wa mule ndani,
Mfanyakazi:habari yako bimkubwa naweza kukusaidia nini?
Bimkubwa:nilikuwa nataka kujua hili gari ni kiasi gani?
Mfanyakazi: We kuligusa Rim tu umejamba je nikikutajia bei si utajinyea kabisa?

0 comments:

Post a Comment