Thursday 11 September 2014

Huyu student ni kiboko

Thursday, September 11, 2014 No comments

JOHN alikuwa analala darasani wakati mwalimu anafundisha!

MWALIMU: We John kwanini unalala wakati mi nafundisha?
JOHN: Unajua mwalimu sauti yako nzuri ndio maana nikalala!

MWALIMU: Sasa mbona wenzako hawajalala?
JOHN: Kwa sababu wao hawakusikilizi!!

MWALIMU: Haya nitajie mifano ya wanyama kumi wa pori...
JOHN: Aaaah! uliza swali lingine bhana hilo siwezi kujibu ni rahisi mno!

MWALIMU: Jibu kwanza hilo kama ni rahisi!
JOHN: Simba saba na Chui watatu...!!!

0 comments:

Post a Comment