Saturday 27 September 2014

Huyu mtoto ni balaa

Saturday, September 27, 2014 No comments

MTOTO : Baba unaweza kumwachia hilo gari lako (V8) house boy/girl akaliendesha? BABA:Siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe kwani nimenunua kwa fedha ghali sana. MTOTO:Je? Mnaweza kumwachia mali zenu house boy/girl zote wazitumie? MAMA:Haiwezekani kumuachia kwa kuwa atatuacha katika hali ngumu ya maisha. MTOTO:Unaweza kumpa houseboy/girl namba yako ya siri ya Bank? BABA:Wewe mtoto wewe unatafuta balaa sasa,Unataka achukuwe pesa zote atuache katika hali ya umasikini sisi hapa. MTOTO:Sasa Wazazi wangu nimeelewa kuwa hamuwezi kuwa kabidhi kitu chochote chenye thamani houseboy/girl? BABA & MAMA:Ndiyo mtoto wetu hatuwezi kuwa kabidhi vitu vya thamani. MTOTO:Sasa kwanini mnanikabidhi mimi kwa houseboy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi jioni kumbe mimi sina thamani kwenu eeee!

0 comments:

Post a Comment